SIMBA WAKWAMA HUKO SHINYANGA WAACHA PENGO DOGO TU DHIIDI YA YANGA>> - LAKE MEDIA TV

Breaking

Music

BANNER 728X90

Thursday, 15 February 2018

SIMBA WAKWAMA HUKO SHINYANGA WAACHA PENGO DOGO TU DHIIDI YA YANGA>>

Mwadui wameisimamisha Simba baada ya kushinda nane mfululizo za ligi kuu Tanzania bara, Mwadui wamelazimisha sare ya kufungana 2-2 kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.



Mbeya City 0-1 SimbaTanzania Prisons 0-1 SimbaNdanda 0-2 SimbaSimba 4-0 Singida UnitedKagera Sugar 2-0 SimbaSimba 4-0 MajimajiRuvu Shooting 0-3 SimbaSimba 1-0 Azam



Simba ndio ilianza kupata goli la kuonoza mapema dakika ya 10 kupitia kwa mshambuliaji wake John Bocco ambaye aliunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Shiza Kichuya.

David Luhende akaisawazishia Mwadui dakika ya 60 kwa mkwaju wa adhabu ndogo akimchungulia moja kwa moja Aishi Manula.



Emanuel Okwi akaifungia Simba bao la pili kwa penati baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Joram Mgeveke kwenye box lakini dakika moja kabla ya mchezo kumalizika Paul Nonga akaisawazishia Mwadui na kuganya matokeo kusomeka Mwadui 2-2 Simba.

Sare hiyo inaifanya Simba kufikisha pointi 42 na kuendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi tano (5) mbele ya Yanga yenye pointi 37 ikiwa nafasi ya pili.



Simba imeshamaliza mechi zake za Kanda ya Ziwa, imecheza ugenini na Kagera Sugar, Mbao, Stand United pamoja na Mwadui FC (wameshacheza mechi mbili) kwa hiyo timu nyingine za Kanda ya Ziwa zitasafiri kuifuata Simba jijini Dar es Salaam.



Bado Simba inaendelea na rekodi yake ya kutopoyeza mchezo wa ligi kuu Tanzania bara. Imecheza mechi 18, imeshinda michezo 12 na kutoka sare katika mechi sita.

No comments:

Post a Comment